Kiongozi wa Kambi rasmi
ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe jana alitangaza orodha ya majina ya
wabunge wa upinzani wanaounda baraza la mawaziri vivuli, huku akimtosa
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Mbowe na Zitto walikuwa
marafiki wakubwa waliozunguka nchi nzima kuijenga Chadema kwa miaka kumi
iliyopita, kabla ya kugeuka kuwa mahasimu wakubwa wa kisiasa ndani ya
mwaka mmoja tu. Chadema walimtuhumu Zitto kwa usaliti na kufikia hatua
ya kumtimua katika chama hicho.
Hata hivyo, uamuzi wa
Chadema ulimpa Zitto akili ya ziada ya kuanzisha chama kipya cha siasa
cha ACT-Wazalendo ambacho kilishiriki uchaguzi Mkuu na kumsimamisha
mgombea urais, Bi. Anna Mghwira na wabunge wengi.
Lakini, kwakuwa siasa
haina urafiki au uadui wa kudumu, katika mkutano wa pili wa Bunge la 11,
Zitto Kabwe, Freeman Mbowe na wabunge wengine wanaounda Ukawa
walionekana kushirikiana kwa karibu kupinga hoja za CCM na kutoka na
msimamo mmoja.
Sio Mbowe peke yake,
hata Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ambaye alikuwa hasimu mkubwa wa
Zitto akimshambulia kwa maandishi kwenye gazeti lake la Mwana Halisi,
alionekana kuwa karibu naye na kushirikiana.
Kadhalika, Mwanasheria
wa Chadema, Tundu Lissu aliyekuwa kinara wa kumtimua zitto Chadema na
kusimamia kesi mahakamani kuhakikisha n Zitto anaondoka katika chama
hicho, alishirikiana naye kwa ukaribu kuomba miongozo iliyowabana
wabunge wa CCM. Hali iliyomuonesha Zitto kuwa ndai ya kundi la wabunge
wa vyama vinavyounda Ukawa.
“Kushirikiana na Zitto
si jambo la ajabu kama ambavyo umeona tukifanya. Yapo majeraha mengi
ambayo tumeyapitia pande zote (Chadema na Zitto) ambayo huwezi kuyatibu
kwa siku moja. Yapo ambayo yatapona kulingana na muda. Unaweza kumfanyia
mtu kitu kibaya, lakini baadaye ukatambua kuwa umekosea. Chochote
katika siasa kinawezekana,” Mbowe alieleza hivi karibuni.
Kutokana na kutomuweka
Zitto kwenye orodha ya mawaziri vivuli, nafasi ambayo Zitto angeweza
kuimudu bila shaka kutokana na uwezo wake kisiasa, Mbowe alilazimika
kueleza sababu na vigezo walivyotumia kumkata.
“Ukawa tulisaini tamko
la pamoja la ushirikiano na hiyo ilikuwa katika Bunge la Katiba. Kumbuka
tumeshirikiana katika Uchaguzi Mkuu na kupata madiwani na wabunge ambao
ndiyo hawa wamezaa baraza hili,” alisema.
“Ushirikiano wetu upo
katika halmashauri na majiji. Kutokana na jambo hilo huwezi kuiingiza
ACT maana haikuwapo katika makubaliano ya Ukawa,” aliongeza Mwenyekiti
huyo wa Chadema.
Pamoja na mambo mengine
yaliyojitokeza Bungeni, Zitto aliungana na Ukawa kupinga kitendo cha
Serikali kutangaza kuwa TBC haitaonesha ‘Live’ baadhi ya vikao vya Bunge
na hata wote waliondoka bungeni na kukaa pamoja kuzungumza na vyombo
vya habari.
Hata hivyo, baada ya Mbowe kutangaza baraza hilo kivuli, Zitto aliwapongeza na kuahidi kushirikiana nao.
Hongera sana dada yangu
@halimamdee kuteuliwa kuwa Waziri Kivuli Fedha na Mipango. Nitakupa
Ushirikiano katika kuisimamia Serikali..
Post a Comment