Siku moja baada ya CCM kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa chama hicho, Pius Msekwa amesema kuna haja ya kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho hasa muundo wa halmashauri kuu ya taifa.
Katika
chapisho lake kuhusu tathmini ya miaka 39 ya chama hicho itakayochapwa
kesho katika gazeti hili, Msekwa amesema mabadiliko hayo yanahitajika
kufanywa kabla ya mwenyekiti wa sasa wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete
kukabidhi kijiti hicho kwa Rais John Magufuli.
Msekwa
ambaye ni katibu mkuu wa kwanza wa Tanu alisema uzoefu unaonyesha
kwamba mageuzi yaliyofanyika kwenye chama hicho mwaka 2011 katika muundo
wa ngazi ya Taifa, hususan wa halmashauri kuu, hayakuleta tija
iliyokuwa imetegemewa.
“Kwa
ajili hiyo, ingefaa sana kama chama kingerejea kufanya mabadiliko
mengine ya muundo wake, ili kumuwezesha mwenyekiti mpya aweze kuanza na
muundo mpya ulioboreshwa,” alisema.
Msekwa ambaye pia ni makamu mwenyekiti mstaafu wa chama hicho alibainisha kuwa muundo huo ulibuniwa katika kipindi cha utawala wa chama kimoja kwa lengo maalumu la kutekeleza sera iliyokuwapo wakati huo ya “chama kushika hatamu za uongozi” wa nchi.
Msekwa ambaye pia ni makamu mwenyekiti mstaafu wa chama hicho alibainisha kuwa muundo huo ulibuniwa katika kipindi cha utawala wa chama kimoja kwa lengo maalumu la kutekeleza sera iliyokuwapo wakati huo ya “chama kushika hatamu za uongozi” wa nchi.
“Lakini
katika hali iliyopo sasa, ni dhahiri kwamba halmashauri kuu ya taifa
imekuwa ni kubwa mno, yenye wajumbe zaidi ya 480... Kwa sababu zote
hizo, inafaa kabisa kwamba chama kitumie fursa hii ya mabadiliko ya
mwenyekiti wake, kufanya mabadiliko ya kupunguza ukubwa wa halmashauri
kuu.”
Mbunge
huyo wa zamani wa Ukerewe alisema athari zake ni kwamba mbali na
gharama kubwa za kuhudumia vikao vyake, wajumbe walio wengi hawafanyi
kazi za chama katika wilaya zao, bali wanatumia muda wao mwingi
kujiandaa kugombea ubunge huku akisema utunzaji wa siri za kikao hicho
muhimu umekuwa mgumu.
Alisema
Katiba ya mwanzo ya CCM, toleo la mwaka 1977 ilikuwa na halmashauri kuu
ya Taifa ndogo tu, na pia kamati kuu ndogo, na haikuwa na kikao cha
sekretarieti kama ilivyo sasa.
Alisema
mabadiliko makubwa yalikuja kufanyika baada ya kupitishwa kwa “Mwongozo
wa CCM wa mwaka 1981” ambao ulikomalia kwelikweli suala la chama
kushika hatamu za uongozi.
Alisema
kutokana na mwongozo wa 1981, kikao cha halmashauri kuu ya Taifa
kilifanywa kuwa kipana na chenye wajumbe wengi kwa kuongeza kundi jipya
la wajumbe 90.
Miongoni wajumbe hao ni wa kamati kuu, sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa na makatibu wa mikoa.
Kuhusu
kamati kuu, Msekwa alisema Katiba ya mwanzo ilikusudia iwe ni kikao
kidogo cha kumshauri mwenyekiti wa chama katika mambo ya uendeshaji wa
shughuli za kila siku.
“Kamati
hii mwanzoni ilikuwa ni ndogo sana, yenye wajumbe 15 tu. Na ndiyo
sababu iliwekewa vikao vya mara nyingi zaidi, ili iweze kutekeleza
wajibu huo kwa ufanisi,” alisema.
Kuhusu
sekretarieti, Msekwa alisema katiba ya mwanzo haikuwa na sekretarieti,
lakini ilikuja kubuniwa baadaye katika vuguvugu la utekelezaji wa sera
ya chama kushika hatamu za uongozi.
Alisema kamati kuu ilifananishwa na Baraza la Mawaziri la Serikali ambalo wajumbe wake lazima watoke miongoni mwa wabunge.
Lakini
alisema, mabadiliko hayo yote yalifanyika katika kipindi cha utawala wa
chama kimoja kwa lengo la kukifanya kionekane dhahiri kwamba kinashika
hatamu za uongozi wa nchi.
Alisema
chini ya mfumo uliopo sasa wa vyama vingi vya siasa, kazi ya kushika
hatamu za uongozi kwa maana ya kusimamia na kuishauri Serikali ni kazi
ya Bunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
“Kwa maneno mengine, msingi wa majukumu ya chama umebadilika kabisa,” alisema.
Akielezea
kuhusu suala la kura za maoni katika chaguzi za ndani ya chama, Msekwa
alisema jambo hilo pia linahitaji kuangaliwa upya. “Hii ni kwa sababu
kuna wasiwasi kwamba kura za maoni hivi sasa zimekuwa ni chanzo kikubwa
cha rushwa ndani ya chama.
Kwa kifupi, faida iliyokusudiwa kupatikana kutokana na utaratibu huu wa kura za maoni kupigwa na wanachama wote, ikawa imepotea. Ndiyo sababu kuna haja ya kuangalia utaratibu huu upya.”
Kwa kifupi, faida iliyokusudiwa kupatikana kutokana na utaratibu huu wa kura za maoni kupigwa na wanachama wote, ikawa imepotea. Ndiyo sababu kuna haja ya kuangalia utaratibu huu upya.”
Post a Comment