Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI AICHARUKIA SUKARI NCHINI


RAIS John Magufuli amesema amedhamiria kwa dhati kufufua viwanda vya ndani na kama mfano amepiga marufuku kwa kiongozi yeyote wa serikali, kutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi zaidi yake.

Aidha, amesisitiza kwamba ataendelea kutumbua majipu ya viongozi mafisadi na wala rushwa, kwa kuwa yeye na viongozi wenzake sio wakatili, ila ni kutokana na nchi kuoza.

Amesema yupo radhi kuchukiwa na Watanzania wachache, ambao wamekuwa wakihusika na vitendo vya ufisadi, vinavyoathiri maisha ya Watanzania wengi ili kuiwezesha nchi kusonga mbele kuelekea kwenye uchumi wa kati kwa kasi.

Rais Magufuli alisema hayo Ikulu Dar es Salaam jana, alipokutana na makundi mbalimbali ya wadau walioshiriki kwenye kampeni zake kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana na kuibuka na ushindi uliomuwezesha kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Akizungumzia ufufuaji wa viwanda ikiwa ni moja ya eneo alilolitilia msisitizo mkubwa wakati wa kampeni, Rais Magufuli alisema nia yake ya kufufua viwanda ipo pale pale na kusema tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa.

Akitoa mfano, Rais alisema wakati yapo maeneo ambayo wakulima wanajishughulisha na kilimo cha miwa na zao hilo kuwa tegemeo lao katika kuinua uchumi wao, wapo wafanyabiashara wanaojali maslahi yao binafsi ambao wamekuwa wakiagiza sukari kutoka nje hatua inayosababisha kufa kwa viwanda vya sukari vya ndani.

“Mtu anaagiza sukari kutoka nje, tena wakati mwingine ni sukari ambayo muda wake wa kuisha matumizi umekaribia kumalizika. 

"Huyu mfanyabiashara anaingiza sukari hiyo na kuifungasha upya ili isijulikane kuwa inakaribia kuharibika na kuwauzia wananchi masikini.

 “Kitendo hiki kinasababisha sukari inayozalishwa na viwanda vya ndani kukosa soko, wakulima wanakosa soko la miwa yao, na serikali nayo inakosa mapato ya ushuru. 

"Kwa vile bahati nzuri Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na Makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan) mpo hapa, nasema kuanzia sasa asiwepo mtu wa kutoa kibali cha mtu kuagiza sukari kutoka nje hadi ruhusa hiyo itoke kwangu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema mkakati kama huo hautaishia kwenye sukari pekee, bali ni mkakati ambao utahusu maeneo yote ya uzalishaji ili wananchi wa kipato cha chini waneemeke na nchi yao. 

“Nimekuwa nasema nchi yetu si masikini. Hii nchi ni tajiri sana, lakini wapo watu wamekuwa wanajinufaisha wao. Wapo tayari wapokee virushwa ili waneemeke wao huku Watanzania wengi wakiumia na kuteseka. 

“Ndio maana nasisitiza kwamba nitaendelea kutumbua majipu ya viongozi mafisadi na wala rushwa.

"Tunapotumbua majipu si kwamba sisi ni wakatili hapana, ila ni kutokana na nchi yetu kuoza. Kila unapotupia jicho pameoza, hadi wakati mwingine unashindwa kuamua uanze na jipu lipi na lipi ulitumbue kesho, yapo majipu mengine hayasikii dawa. 

“Hawa watu wanaolalamika sana sasa ni wachache ambao walikuwa wananufaika na ufisadi na rushwa. Ni bora ukachukiwa na watu 1,000 ili upendwe na watu milioni 50.Kama nitaboresha maisha ya Watanzania milioni 50, hata kwa Mungu tutapokelewa,” alisema Rais Magufuli.

Alisema serikali yake itaendelea kuchukua hatua katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya neema na ya uchumi wa kati na kuwa umoja, mshikamano na uzalendo usioambatana na tofauti za kidini, ukabila na itikadi za kisiasa ni nyenzo kubwa katika kufikia mafanikio hayo.

==>Tazama  Video  hii  kumsikiliza  Rais  akitoa  amri  ya  kupiga  marufu  uagizaji  Sukari
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top