Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SASA MAMBO SHWARI MUHIMBILI

hi1
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi, Aksante wakati akimwelezea juhudi zinazoendela za kukarabati jengo la watoto ambalo lipo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Pombe Magufuli alivyoagiza. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mkururugenzi huyo. Leo Waziri Mwalimu na naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Kigwangalla wametembelea Jengo la Watoto na Jengo namba mbili la wazazi kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye ametaka jengo la watoto linalovuja likarabatiwe haraka.
hi3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Professa Lawrence Mseru akifafanua jambo mbele ya Waziri Mwalimu na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dk Kigwangalla kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilolitoa hivi karibuni.

hi4
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla wakitazama jengo (pichani halipo) ambalo limeaanza kukarabariwa baada ya agizo la rais.

hi5
Waziri Ummy Mwalimu na naibu waziri wake, Dk Kigwangalla wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali (MNH), Professa Museru katika wodi ya wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto ambalo limeanza kukarabatiwa.
hi6
Waziri Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto.
hi7
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa watoto wanaougua ugonjwa wa saratani waliolazwa katika jengo la watoto lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Picha zote na John Stephen-Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
…………………………………………………………………………………………………
Na Neema Mwangomo-PRO- MNH
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto  Ummy  Mwalimu leo  ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- kwa lengo la kukagua jengo la watoto pamoja na jengo la wazazi namba mbili ( Maternity Block Two)  ili kuona utendaji kazi na  utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli .
Mwishoni mwa wiki iliyopita,  Rais Magufuli aliagiza watumishi wa Wizara  ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , wazee na Watoto kitengo cha  afya ya mama na mtoto kuhama katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili kulitumia kama wodi ya wazazi .
Waziri Ummy  ambaye ameambatana na Naibu Waziri Dokta Hamis  Kigwangala ameelezea kuridhishwa na ukarabati unaoendelea katika majengo hayo  .
“Jengo la watoto tatizo kubwa lilikuwa  ni miundombinu ya maji lakini naona ukarabati unaendelea vizuri na nina imani kuwa ukarabati utakamilika kwa wakati” amesema Waziri .
Akizungumzia kuhusu jengo la wazazi namba mbili , Waziri huyo wa afya amesema kuwepo kwa jengo hilo ni faraja kwa kina mama  na kusisitiza kwamba hakuna mama mjamzito atakayelala chini .
Mpaka sasa kina mama 53 tayari wamehamia  katika jengo hilo na wanapatiwa huduma zote.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top