Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SIMU FEKI ZAWA GUMZO

Wakati tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya wafanyabiashara za simu za mikononi katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam walalamikia kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki huku watuamiaji nao wakilalamikia kuwa watakosa mawasiliano kutokana na simu origino kuwa ghali.

Siku chache baada ya mamalaka ya mawasiliano nchini TCRA kuonesha msimamo wake wa kuzifungia simu hizo baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wameelezea kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukosa wateja na hivyo kusababisha hata simu ambazo sio feki kukosa wateja na kubaini kupata hasara kubwa kutokana na azimio hilo ambapo wameziomba mamlaka husika kuongeza muda ili kuwapa nafasi ya kujipanga ili kutafuta mtaji wa kuingiza simu zinazotakiwa.

Baadhi ya watumiaji wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.

Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kuzima simu feki na walikuwa na haya ya kusema.

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayri imeonesha msimamo na kutangaza kuwa tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki zitazimwa ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari wameshazifungia kabisa simu feki.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top