Baada ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kamera ya Binagi Media Group imenasa picha za daraja hilo litakavyokuwa baada ya kukamilika hivyo enjoy kuzitamaza na uvute picha namna Mwanza inavyoendelea kuboresha miundombinu yake.
Ukifika Mwanza, Make Sure unafika Rock City Mall Mwanza.
Tazama HAPA DARAJA LA MABATINI
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Post a Comment