Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TUMBUA MAJIPU YAWALIZA WAUZA MITUMBA

ZOEZI la kuwabana wafanyabiashara wakwepa kodi  sambamba na kuwawajibisha watumishi wa umma wanaokwenda kinyume na majukumu yao, maarufu kama kutumbua majipu, linawaliza wauza mitumba kutokana na kupandishiwa bei inayowafanya nao wapandishe kwa wateja wao.

Mmoja wa wauzaji maarufu wa nguo za mitumba,Pius Rutta ‘Mzee wa Pamba’ (pichani) anayefanya shughuli zake Makumbusho jijini Dar es Salaam, alisema tumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli, inawafanya wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakikwepa kodi na hivyo kuuza ‘mabelo’ kwa bei rahisi, sasa kuuza kwa bei ya juu baada ya kulazimika kulipa kodi.

“Tangu Magufuli alipoingia madarakani na kuwabana wote waliokuwa wakikwepa kulipa kodi hali imekuwa mbaya, kama unavyoona watu wanaokuja kununua nguo siyo wengi kufuatia bei kuwa kubwa,” alisema.

Mzee wa Pamba alisema jambo hilo limewafanya wawe katika wakati mgumu kibiashara kwa sababu nguo zimepanda sana bei tofauti na zamani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top