Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAMACHINGA WAMUUA TAJIRI KWA MAWE DAR.... KISA NYANYA






 

Watanzania tunaelekea wapi? Wamachinga wamuua tajiri kwa mawe Dar... Kisa NYANYA.....Habari na Picha
By Makongoro Oging’, 
DAR ES SALAAM: 
Mfanyabiashara mkubwa wa
Kariakoo jijini Dar, Stephen Elija
Silas (27) ameuawa kwa kupigwa
mawe na wafanyabiashara
wadogowadogo ‘Wamachinga’ kwa
madai ya kukanyaga kwa gari
lake nyanya walizopanga
barabarani, Uwazi limefuatilia.
Tukio hilo lenye simulizi ya
kusikitisha lilijiri usiku saa nne ya
Februari 8, mwaka huu katika
makutano ya Mtaa wa Msimbazi
na Aggrey, Kariakoo jijini Dar es
Salaam wakati marehemu huyo
alipokuwa akilikwepa gari
lililobeba maziwa.
Marehemu Stephen alikuwa
akiendesha gari lake aina ya
Toyota Corolla lenye namba za
usajili T 312 AZU ambalo pia
lilipondwa kwa mawe na
Wamachinga. Alikuwa njiani
kuelekea nyumbani kwake,
Kinondoni, Dar.
MBALI NA MAWE, ALICHOMWA
KISU
Taarifa zaidi zinadai kuwa, mbali
na marehemu huyo kupigwa
mawe, pia Wamachinga hao
walimchoma kisu kwenye kwapa
la mkono wa kulia akiwa ndani
ya gari.
SHUHUDA ASIMULIA
Mmoja wa mashuhuda wa tukio
hilo ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini alisema
marehemu alikuwa akitokea
upande wa uliyokuwa mzunguko
wa Shule ya Uhuru, akaingia
Barabara ya Msimbazi. Alipofika
makutano ya mtaa huo na Aggrey,
mbele yake kulikuwa na gari
lililobeba maziwa ambalo
liliyumba, hivyo ili asiligonge
akalikwepa na hivyo kujikuta
akikanyaga kwa bahati mbaya
nyanya za Wamachinga hao
ambao palepale walianza
kumshambulia kwa maneno,
baadaye mawe na kumalizia na
kisu.
WALICHANGANYIKA NA WAHUNI
“Jitihada za wasamaria wema
kumuokoa zilishindikana licha ya
jamaa kuomba msaada. Mimi
naamini kuwa, mbali na
Wamachinga pia wahuni wa
mitaani walikuwepo kwa lengo la
kupora vitu vyake,” kilisema
chanzo hicho.
ALIOMBA MSAMAHA
Chanzo: “Kwanza jamaa
alipobaini amekanyaga nyanya za
biashara ya Wamachinga
hakufanya fujo kwa kunena
mabaya, aliomba asamehewe au
alipe fedha kulingana na nyanya
zilizoharibika lakini Wamachinga
na wahuni hao hawakumsikiliza,
waliendelea kumwadhibu.
“Kulikuwa na wananchi
waliokuwa wakitokwa machozi
walipomuona jamaa akipigwa
mawe kwa kosa ambalo halina
kichwa wala miguu.”
WANANCHI WAPIGA SIMU
POLISI
Inaelezwa kuwa, baadhi ya
wananchi waliamua kupiga simu
Kituo cha Polisi Msimbazi ili
wakamuokoe Stephen lakini licha
ya kuwahi katika eneo la tukio,
walimkuta akiwa hoi kutokana na
kipigo na alifariki dunia wakati
polisi wakimkimbiza Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa matibabu.
UWAZI LAFIKA MSIBANI
Uwazi kama ada yake, lilifika
kwenye msiba wa Stephen, kwa
baba yake mkubwa marehemu
aitwaye Charles Losaru, Mtoni
Kijichi jijini Dar na kuzungumza
na mdogo wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina la
Rebeca Elija ambaye alisema
alikuwa na marehemu muda
mfupi kabla ya kifo chake.
Alikuwa na haya ya kusema:
“Marehemu kaka Stephen
alikuwa mfanyabiashara mwenye
maduka ya bidhaa mbalimbali,
Kariakoo na Sinza. Huwa ana
kawaida ya kutusindikiza na gari
lake baada ya kufunga maduka.
Mimi na ndugu zangu wengine
tunaishi Kitunda yeye Kinondoni.
Amekuwa akitusindikiza hadi
Banana na kutuacha tupande
daladala.
“Siku ya tukio, alitusindikiza na
kutuacha Buguruni. Ilikuwa saa
tatu usiku. Ni sisi tuliamua
atuache hapo badala ya Banana.
Yeye akarudi akipitia Kariakoo
kwa vile kuna ndugu zetu
wengine wana maduka maeneo
hayo.”
SIMU YAKE YAPIGWA, YAITA TU!
Rebeca anaendelea: “Tuliposhuka
kwenye daladala pale Banana,
nilimpigia simu mara tatu ikawa
inaita bila kupokelewa.
Nikampigia simu mchumba wake,
anaitwa Neema William ambaye
ilikuwa wafunge ndoa hivi
karibuni. Nilitaka kujua kama
kaka alishafika nyumbani, Neema
akasema hajafika.
TAARIFA ZA KIFO KWA NDUGU
“Sasa wakati tunapanda daladala
Banana kwenda Kitunda,
nilipigiwa simu na marafiki zake
na kuniambia kuwa Stephen
amepata matatizo yupo
Muhimbili. Niliposhuka Kitunda,
alinipigia simu kaka yangu
mkubwa, anaitwa Silas ambaye
tulikuwa naye Kariakoo,
akaniambia kaka amefariki dunia
(machozi).
“Kaka Stephen alikuwa mpole
kupita kiasi! Hivi ni kwa nini
walimuua kikatili vile? Kwanza
pale walipompigia mawe, mbona
ni sehemu ya magari na wala si
pa kupanga nyanya wala bidhaa
nyingine. Inaniuma sana (machozi
tena).”
MAREHEMU AAGWA DAR,
AZIKWA ARUSHA
Mwili wa marehemu Stephen
uliagwa Alhamisi ya wiki iliyopita
katika Kanisa la Anglikana lililopo
Muhimbili na kusafirishwa
kwenda nyumbani kwao, Daraja
Mbili mkoani Arusha kwa mazishi
yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.
POLISI WAZUNGUMZIA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Ilala, ACP Ernest Matiku
alipohojiwa na Uwazi ofisini
kwake wiki iliyopita, alikiri
kutokea kwa tukio hilo na
kueleza kuwa, marehemu
alipigwa na kundi la watu baada
ya kugonga gari lililokuwa likiuza
maziwa kisha kukanyaga bidhaa
za Wamachinga zilizokuwa
zimepangwa chini.
Gari likiwa limehalibika vibaya.
“Mpaka sasa tunawashikilia watu
kumi kutokana na tukio hilo na
bado upelelezi unaendelea. Kwa
sasa hakuna biashara ya
Wamachinga inayoendelea
maeneo yale ya Mtaa wa
Msimbazi.
“Nalaani kitendo kile cha mauaji
kwani hata kama marehemu
alifanya kosa lakini sheria zipo na
siyo kuchukua maamuzi hayo
mazito ya kukatisha maisha ya
binadamu, wote waliofanya
unyama ule watashughulikiwa
kisheria upelelezi ukikamilika,”
alisema kamanda huyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top