Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI KAIRUKI ATUMBUA MAJIPU VIGOGO


WAZIRI  wa nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi  wa Umma na Utawala bora,Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro kutoka na uzembe ulioisababishia serikali  hasara  ya  bilioni 1.
 
Vilevile Waziri Kairuki amewasimamisha  kazi Mkuu wa chuo hicho tawi la Dar es salaam,Joseph  Mbwilo na Silvanus  Ngata ambaye naye ni Mkuu wa chuo hicho tawi la Tabora.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Waziri Kairuki amesema amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya kubainiutendaji usioridhisha katika vyuo hivyo.
 
Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika  chuo hicho.
 
“Mwaka  2011 hadi  2013 bwanaSilvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo hicho tawi la Mtwara tofauti na fedha iliyokuwa imepangwa.  

"Chakushangaza, huyu Nassoro ambaye ni mkuu wao,  baada ya kugundua kosa hilo alishindwakumuwajibisha na badala yakealiamua kumhamishia tawi la chuo cha Tabora. Sasa mimi nawasimamisha kazi wote ."Amesema Kairuki
 
Pia waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo.
 
“Huyu Mbwiro kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi  kiasi cha bilioni 1 ,lakini licha ya ubadhilifu huo, Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa fedha."Alisema Waziri Kairuki.
 
Wakati Waziri Kairuki akitumbua majipu hayo,mmoja wa watendaji hao,Said Nassoro alikuwepo kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top