Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WAZIRI wa
Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.
Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande wamekutana kwa
ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe
Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na
uendeshaji wa kesi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji
Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyon
itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili
wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.
Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya
ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa
ambayo hazina mahakama kuu.
Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha
wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe
kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.
Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa
hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya
mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.
Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe
amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili
wananchi waweze kupata haki.
Amesema hatua za ujenzi wa Mahakama ya Wahujumu Uchumi na Wala
Rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili
uboreshaji wa miundombinu ya mahakama.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akimshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake
ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3
zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya
katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria
Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
(kushoto).
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu Serikali kuendelea
kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ili kuwezesha ufanisi wa shughuli
zake.
Post a Comment