TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumekuwa na minongono mingi kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu Filamu ya Mapenzi ya Mungu ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos Nchini Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA).
Ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya Mungu ni Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani ana haki zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo.
Filamu ya Mapenzi ya Mungu imetengenezwa chini ya kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.
IMETOLEWA NA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Post a Comment