Haya hapa ndio madai 8 ya wanafunzi wa Chuo cha St.Joseph tawi la Dar yaliowafanya waandamane jana kuelekea Wiza ya Elimu kuwasilisha madai yao lakini hata hivyo maandamano hayo yaligonga mwamba baada ya wanafunzi hao kutimuliwa na FFU.
MADAI 8 KUTOKA KWA WANAFUNZI HAO WANATAKA MADAI HAYA YA FIKE KWA WAZIRI WA ELIMU.
- Baada ya kufungwa kwa campus ya Arusha education ambayo ni main campus na songea kwa nin wameiacha campus ya luguruni kwa faculty ya education wakati Arusha ndio kichwa.
- Kuwepo kwa faculty ya education kwa tawi la luguruni kisirisiri bila kuwa na uhakika wa manzingira ya wanafunzi.
- Kutofundishwa kwa kufuata mitaala ya Tanzania ikiwa ajira tunatafuta nchini mwetu...kwa faculty ya education..hakuna mwalimu wa kihindi aliye na taaluma ya ualimu ambaye anafundisha wanafunzi.
- Ada kubwa mno kupita maelezo ambayo haifanani na maisha ya chini ya mtanzania kama inavyosema Sera ya CHUO...haswa sis wanafunzi wa education.... Ada sh..1,850,000.
- Sababu zilizo vifanya vyuo vya Arusha(edu-main campus) na Songea ndizo tulizonazo hapa Dar. Hivyo hakuna sababu ya kulifumbia macho hili swala la kuidhinisha kuwepo faculty ya education kwa tawi la Luguruni.
- Elimu ni hazina isiyoharibika hatutaki kuharibu kizazi chetu kwa kuwarithisha elimu mbovu ni bora kulitumbua jipu hili kabla halijatuumbua.
- Tunamuomba muheshimiwa waziri wa elimu mama yetu mpendwa aingilie kati swala hili maana yeye aliyebaki kufanya mapinduzi ya kielimu Tanzania.
- Mwisho kwa taarifa iliotumwa sio ya kweli kwamba. Tunataka CHUO cha Arusha kifunguliwe sio kweli tunataka kujua kwa nin wametuacha Education tawi la dar kulingana na sababu hizo tajwa hapo juu
Post a Comment