Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeweza kukusanya shilingi bilioni 4.3 kufikia mwezi Januari 2016 tofauti na makusanyo ya nyuma yaliyokuwa bilioni 2.6 kwa mwaka 2015.
Baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa awamu ya Tano nchini Dkt. John Magufuli katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili imeiwezesha Hospitali hiyo kukusanya shilingi bilioni 4.3 kufikia mwezi Januari 2016 tofauti na makusanyo ya nyuma yaliyokuwa bilioni 2.6 kwa mwaka 2015.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Laurence Muselu kwenye mazungumzo maalum na East Africa Radio na kuongeza mikakati waliyojiwekea imeanza kuzaa matunda ambayo ni maalumu kwaajili ya kuwasaidia watanzania wote bila kuwabagua.
Prof. Muselu amesema kuwa uongozi wa hospital hiyo umeyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na wagonjwa waliofika hospitalini hapo kwaajili ya kupatiwa huduma mbalimbali na kuhakikisha kila mfanyakazi anafanya kazi kwa kutimiza malengo waliyokubaliana sambamba na kuwalipa malimbikizo mbalimbali watumishi wa hospitali hiyo.
Loading...
Post a Comment