Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HUKU MWANAYE AKITUMBUA MAISHA .... BABA YAKE DIAMOND ASHINDA NJAA

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.


Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia  shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.

 Familia ya Diamond Platnumz ‘wakitumbua’ Ulaya.

“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa  kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”

MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.

 Mzee Abdul Juma.

HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

 “Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100  na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.

DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.

“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho;

DIAMOND ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.
Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.

Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top