Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu".
Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-15 Machi, 2016
Post a Comment