Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

"Kamata weka ndani" - Rais Magufuli

RAIS John Magufuli amewawataka Wakuu wa Mikoa nchini kukamata watendaji wa kata wanaowavuruga wananchi na kuwaweka ndani ili kuwatia adabu, anaandika Faki Sosi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwaapisha viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili baada ya kuwateua.

“Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka ndani hata masaa 48, wawekeni ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa,”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, ameonesha kukerwa na tabia ya vijana kutofanya kazi na badala yake kuwa mitaani wakicheza na kwamba, wakuu hao wa mikoa wasimamie hilo.

“Kwa kweli ni aibu kuona kijana saa mbili au tatu asubuhi anacheza PoolTable halafu wazee wanalima, kamata peleka kambini walime kwa nguvu,” amesema.

Pia Rais Magufuli amewataka kuwaondoa wafanyakazi hewa kwenye halmashauri zote nchini.
“Mmekula kiapo rasmi nawapa siku 15 kuanzia sasa kuhakikisha wafanyakazi hewa wanaondolewa serikalini mara moja.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top