Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua kikao cha Kamati Kuu Maalum kilichofanyika kwenye Afisi Kuu za CCM Zanzibar,Kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ,Rais wa Srikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ai Mohamed Shein (kulia) wengine pichani ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar) Mhe. Vuai Ali Vuai.
Spika wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Kificho akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakipitia agenda muhimu ya kikao hicho cha Kamati Kuu Maalum ambacho kililenga kupendekeza jina la Spika la Baraza la Wawakilishi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Jerry Silaa muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu Maalum mjini Zanzibar.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakipitia ajenda ya kikao hicho cha Kamati Kuu Maalum, kulia ni Mhe. Pandu Ameir Kificho mjini Zanzibar.
Loading...
Post a Comment