Picha za ujio wa Makatarsi na huyo anayeonekana hapo ni Mkurugenzi wa ZEC Salim Kassim Ali akitoa maelezo ya kuwasili kwake uwanja wa ndege Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imendelea na msimamo wake wa kuhakikisha kwamba vyama vyote vinashiriki katika uchaguzi wa marejeo unatarajiwa kufanyika march 20 mwaka huu.
Hayo yamedhihirikia leo pale ZEC waliupopokea makaratasi ya kupigia kura kutoka Afrika ya Kusini yakiwa yamechapishwa ikihusisha wagombea woote hata wale ambao waliomba kuondolewa katika karatasi hizo kwa madai kwamba uchaguzi huo si halali.
Akizungumza na waandishi baada ya kupokea karatasi hizo Mkurugenzi wa Tume hiyo Salim Kassim Ali aliweza kuonesha mfano wa karatasi hizo ambazo hata Chama kikuu cha Upizani CUF kilichopiga kelele mara kwa mara nacho kimeorodheshwa .
“Wagombea ni walewale waliokuwa katika uchaguzi uliopita ambao waliteuliwa tarehe 6 september 2015 na kama mnavyoona karatasi zetu za mfano” alisema Ali.
Alisema kujiondoa kuna taratibu za kisheria ambazo hazikufuatwa kuda kutokana na hilo wamefanya uchapishaji ule ule wa mwaka jana.
Alisema kilichobakia sasa karatasi hizo ni kuzipeleka kwenye ghala la kuhifadhia karatasi hizo hadi hapo Tarehe 17/03/2016 ambapo zitaaza kusambazwa katika vituo.
Alisema tarehe 18 mwezi huu wataaza kuzipeleka kisiwa cha Pemba na 19 ni katika vituo vyote vya Unguja.
Ali alieleza kwamba wamechapisha makaratasi hayo kulingana na Idadi ya wapiga kura wote ambao wameorodheshwa katika Daftar la wapiga kura Zanzibar ambao ni 503850.
“Tutahakisha mara hii karatasi zoote zimefika mapemaa sanaa ili kuondoa matatizo ambayo yailiweza kujitokeza katika chaguzi zilizopita” alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wa gharama za uchapishaji na usafiri muhasibu wa ZEC Yusouf Ali Hassan alisema mara hii wametumia Ud250000 kiasi ambacho ni kidoogo kulingana uchaguzi uliopita kwa tofauti ya Dola 50000.
Alifahamisha kwamba ghara zote hizo ziliweza kutolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila ya mkopo wowote.
“Tulilipa kwa awamu 60% na ilipokamilika kazi ya uchapisha tumemaliza kilichabakia na kwa maana hiyo hatudaiwi” alisema Hassan.
Akizungumza kiwanjani hapo mwakilishi wa chama cha TADEA Rashid Mchenga alisema anaishukuru ZEC kwa kufanya mambo yao kwa wakati. Alisema wao watashiriki kifua mbelee na hana wasiwasi katika uchagfuzi huo.
Ikumbukwe kwamba vyama zaidi ya 10 viliaandikia ZEC vikiomba kuondolewa katika katasi hizo lakini mambo yamekwenda kinyume chake na sasa majinan na picha yataonekana vile vile.
Vyama vyoote 14 ambavyo vilishiriki uchaguzi 25 October 2015 ndivyo vile vile ambavyo vimechapishiwa makaratasi ya kupigia kura.
Vyama ambavyo vitashiriki ni ACT Wazalendo, ADA-TADEA, ADC, CCK, CCM, CHAUMA, CUF, DP, JAHAZI ASILIA, MAKINI, SAU na TLP.
Post a Comment