Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila akizungumza na wandishi wa haari (hawapo picha) juu ya Wizara inatoa wito kwa wadau wote katika ngazi zote kushirikiana kwa pamoja katika jitihada za kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John.
Wandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,kwa Niaba ya Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kaimu Katibu wa Wizara hiyo, Michael John, amesema kuwa serikali imeweka nguvu zaidi katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema fedha hizo zimetumika katika kuunda tume mbalimbali katika kutoa elimu juu ya ugonjwa,vifaa pamoja na vitanda katika hospitali ambazo zilipatwa na wagonjwa wa jamii hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu amesema Mikoa ya Kanda Ziwa imekuwa na imani potofu juu ya kuchemsha maji ya kunywa kwa kudai kuwa ugonjwa huo unatokana na hali ya hewa pamoja na wavuvi wa kanda hiyo kuwa wakinywa maji yaliyochemshwa wanazma katika mitumbwi yao au wasiweze kuvua samaki hizo.
Amesema ugonjwa wa wa kipindupindu hapa nchini umedumu kwa takribani miezi saba (7) sasa tangu uanze mwezi Agosti, 2015.
John amesema hadi kufikia Machi 13 mwaka huu jumla ya watu 18,399 wameugua ugonjwa huo, kati yao watu 292 wamepoteza maisha.
Takwimu za ugonjwa huu pia zinaonyesha kuwa mikoa ambayo ilikwishakupata ugonjwa imeongezeka na kufikia 23 baada ya Mkoa wa Mtwara kuripoti wagonjwa wawili kuanzia jana ya machi 13 katika wilaya ya Masasi.
Mikoa ya Njombe na Ruvuma ndio pekee hapa nchini ambayo bado haijaripoti mgonjwa wa Kipindupindu.
Takwimu za wiki iliyopita kuanzia tarehe 7 hadi 13 Machi 2016 zinaonyesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imeongezeka ambapo idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hiyo ni 758
Ikilinganishwa na 544 wa wiki iliyotangulia ya tarehe 28 Februari hadi 6 Machi ambapo ni ongezeko la asilimia 40. Mkoa wa Iringa ambao haukuwa umeripoti wagonjwa wiki iliyotangulia, wiki hii imeripoti
Ugonjwa katika Halmashauri ile ile ya Iringa, ambayo bado imeendelea kuripotiwa ugonjwa wa kipindupindu pia imeongezeka kutoka 10 hadi 12. Mikoa hiyo inaongozwa na Morogoro (196), Dodoma, (142), Mwanza(108), Mara(86), Manyara(77), Iringa(77). Mikoa mingine ni pamoja na, Dar es salaam(42), Mbeya(16), Arusha (10),Lindi (2), Mtwara (2) na Rukwa (2).
Post a Comment