Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu.
Dar es Salaam: Mwisho wa malumbano! Tofauti na inavyodaiwa kuwa staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikiuka maagizo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kutoka nje ya nchi kufuatia kesi inayomkabili ya kifo cha mwigizaji Steven Kanumba, Ijumaa Wikienda limechimba ukweli.
Hivi karibuni Lulu alikwenda nchini Nigeria kuhudhuria Tuzo za African Magic Viewers Choice (AMVCA) aliibuka mshindi wa Mtayarishaji wa Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu).
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa makarani wa mahakama hiyo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji wa mahakama hiyo alisema kuwa mawakili wa Lulu walimuombea kibali cha kwenda Nigeria na kupewa kwani walitoa hoja za msingi ikiwemo kwenda kuwakilisha taifa nchini humo.
Kwa upande wake Lulu alisema kuwa hakutaka kuwajibu waliokuwa wakisema kuwa alikiuka maagizo ya mahakama hiyo kwani haruhusiwi kusema lolote zaidi ya kuwaachia mawakili wake ndiyo wenye jukumu hilo.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa mawakili wa Lulu, Peter Kibatala ambaye alisema kuwa walifuata utaratibu zote ndipo mahakama ikatoa kibali kwa hoja kwamba alikuwa anakwenda kuliwakilisha taifa
Post a Comment