Msanii mahiri nchini anaeipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi Nassib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz, amemkumbusha Rais Magufuli kuhusu ahadi yake ya kushughulikia kujenga ukumbi wenye hadhi ya kimataifa ambao utaweza kuruhusu kufanyika shughuli mbalimbali za kimuziki.
Akizungumza na kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds FM Diamond Plutnumz amesema aliwahi kupiga story na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli na kumuomba kupitia serikali yake aweze kuwajengea ukumbi mkubwa wasanii utakao wasaidia kupanua wigo wa muziki nchini kwa shughuli za kimataifa kama tuzo kubwa kufanyikia nchini.Magufuli na Wasanii
Diamond amezidi kueleza kuwa amewahi kuambiwa na baadhi ya waandaaji wa tuzo kuwa wanampango wa kuja kufanyia tuzo nchini Tanzania lakini tatizo hakuna ukumbi mkubwa wa kumudu tukio hilo la aina yake, hivyo Diamond amemuomba Rais Magufuli asiwasahau atimize ahadi yake, ili tasnia ya muziki izidi kusonga mbele.
Post a Comment