Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Kutokana na muda mrefu kutajwa kuwa ni mwanachama wa Freemason, staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kusema kuwa hajawahi kujiunga ila kama kuna mtu anajua kama kweli kuna fedha yupo tayari kuunganishwa.
Akipiga stori na paparazzi wetu, Nay alisema mara nyingi amekuwa akionyesha na kuzitumia alama za freemason kwa sababu anazipenda lakini siyo kwamba ni mwanachama wao ila kama kuna mtu mwenye ufahamu vizuri namna fedha zinavyopatikana huko, yupo tayari kuunganishwa kwani anahitaji fedha zaidi.
“Siko freemason na sijui wanapatikana wapi, nimekuwa nikitumia alama zao hata kwenye video za nyimbo zangu kwa sababu tu nazipenda sana, lakini siyo vinginevyo,” alisema Nay.
Kwa upande mwingine Nay alisema sasa ameamua kubadili staili ya maisha baada ya kupitia kwenye misukosuko mingi ikiwa ni pamoja na gari lake kuvunjwa vioo na kutishiwa maisha kwenye simu na sehemu mbalimbali anazopita.
“Namshukuru sana mama yangu kwani amekuwa akinipigia kelele kila wakati kuhusu kubadili mwenendo wa maisha yangu, kwa mara ya kwanza nimeenda kanisani baada ya kukaa kwa miaka kumi na moja bila kukanyaga kwenye jengo hilo takatifu, hivyo naomba watu wasinifikirie vibaya,” alisema Nay
Post a Comment