Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TUNDU LISSU AFUNGUKA MAZITO

Mwaka 2010 tulishinda ubunge majimbo ya Maswa Magharibi na Mashariki, Bukombe na Meatu, Ilemela, Nyamagana na Ukerewe na Biharamulo na Musoma Mjini.

Yote haya yako Kanda ya Ziwa. Mwaka jana tumeyapoteza yote isipokuwa Ukerewe. Swali ni je, tuliyashinda kwa sababu ya Mh. Mbowe na, kwa hiyo, tumeyapoteza kwa sababu yake??? Tumeshinda Tarime Mjini na Vijijini, Bunda Mjini, Serengeti na Bukoba Mjini, yote katika Kanda hiyo. Je, huko tulikoshinda Mbowe alipeleka nguvu kubwa kuliko tulikoshindwa???.

Kuhusu Lowassa, takwimu za Tume zinaonyesha alipata kura milioni 6 au 40% ya kura zote. Mwaka 2010 Dr. Slaa alipata kura milioni 2.2 au 27% ya kura zote. Nani kati ya wawili hawa anaaminika zaidi na waTanzania kama kura ni kielelezo cha uungwaji mkono??? Nani alikuwa mgumu kuuzwa kwa wapiga kura hapa???.

Tatu, nani aliyemuondoa Dr. Slaa CHADEMA na nani hasa aliyemleta Lowassa. Ushahidi ulioko hadharani na ambao haujakanushwa ni kwamba Dr. Slaa alishiriki katika kila hatua ya kumleta Lowassa CHADEMA.

Alipofanikisha kazi hiyo akakimbia chama na kwenda kumtumikia kafiri. Sasa anaishi ughaibuni Canada na haijulikani kwa gharama za nani. Mwisho, Magufuli ametengua maamuzi kuhusu Tegeta Escrow na kuwarudisha kazini Prof. Muhongo, Change, n.k. Anayedai hatuna agenda ya ufisadi avute subira ili apate kheri.
Tundu Lissu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top