WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kutafutwa kwa Ofisa Ardhi wilayani Busega aliyetoa hati na kibali cha kumuuzia Mtanzania mmoja mwenye asili ya Asia majengo yaliyokuwa yakitumiwa kwa ujenzi wa barabara ambayo yaligeuzwa shule.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu, Waziri Mkuu ameanza kusaka majipu kwa kuagiza kusakwa kwa mtumishi huyo wa umma.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni, majengo hayo yaliyokuwa yakitumiwa na kampuni ya ujenzi ya SK Investment Company Limited, yamebadilishwa hati na kuuzwa kinyemela kwa mtu aliyemtaja kuwa ni Mtanzania mwenye asili ya Asia.
Dk Chegeni alisema majengo hayo yalikuwa yakitumika na yanaendelea kutumika kama shule ya sekondari.
Akizungumzia sakata hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kusakwa kwa ofisa huyo ili aeleze kwa nini alitoa kibali na hati hiyo kinyume cha taratibu.
“Wacha hilo la mahakama likamilike, lakini huyu ofisa ardhi aliyetoa kibali na hati ya kumilikisha aradhi hiyo kwa Mhindi, asakwe ili aje aeleze nani amempa mamlaka hayo ya kutoa kibali na hatimiliki,” aliagiza Waziri Mkuu.
Post a Comment