HILI NI GARI YA Marehemu Sokoine aliyopata nayo ajali katika eneo la Dakawa Mkoani Morogoro tarehe 12 Aprili 1984 wakati akirejea Dar es Salaam kwa barabara akitokea Dodoma ambako alikuwa akihudhuria Bunge.
Wakati Tanzania leo ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 34 ya Kifo cha waziri mkuu Edward Moringe Sokoine wananchi wametakiwa kuunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kupambana na Vitendo vya rushwa na Ufisadi ambavyo vilikuwa vikitekelezwa na kupewa kipaumbele na kiongozi wakati wa uhai wake.
Wakizungumza jiji dsm baadhi ya wananchi wamesema vita dhidi ya wala rushwa,mafisadi pamoja na wabadhilifu wa mali za umma iliyokuwa ikifanywa na marehemu sokoine iliweza kuleta heshima pamoja na kurejesha misingi ya maadili kwa watumishi wa umma.
Aidha wananchi hao wamempongeza rais john pombe magufuri na kumfananisha na Sokoine katika azma yake ya kupambana na ufisadi,Rushwa pamoja na uwajibikaji katika utumishi wa Umma.
Hayati Mwalimu Julias Nyerere akiwa mbele ya maiti ya sokoine..
Post a Comment