Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSANII BONGO MOVIE WOLPER ATIMULIWA NDANI YA NYUMBA, AFUNGASHIWA VIRAGO VYAKE

W3
Jacqueline Wolper
Stori: WAANDISHI WETU
DAR ES SALAAM: STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ambaye hivi karibuni ameonekana kulegalega amedaiwa kutolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Mikocheni jiji Dar.
Chanzo chetu makini kabisa kinadaiwa kuwa kipindi staa huyo akiwa nchini Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini kwa kushindwa kulipia kodi kwa kipindi kinachotakiwa, kabla hata hajarejea mwenye nyumba aliamua kutoa vitu nje na ndugu wa staa huyo kila mmoja kuelekea anakokujua.
“Maskini, wakati Wolper yupo Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini ilishindikana kulipa kodi hivyo mwenye nyumba aliwatimua ndugu zake,” kilisema chanzo hicho.
Kilizidi kufunguka kuwa, baada ya Wolper kurejea nchini ilibidi kuishi hotelini mpaka sasa ili kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kupanga nyumba ambayo ataweza kuishi pamoja na ndugu zake.
“Wolper na mpenzi wake tangu waliporejea nchini wanaishi hotelini, nafikiri wanajipanga ili waweze kupata fedha za kuweza kupanga tena nyumba kama ilivyokuwa huko nyuma,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Wolper kwenye simu ambapo alipoulizwa kama ni kweli ametolewa vitu nje, alijibu;
“Hao wanaosema nimefulia hadi kutolewa vitu nje ni wazushi tu, hawana nia njema na mimi, najua ninachokifanya mjini hivyo hawanipi shida, wache waseme mpaka wachoke.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top