Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NYUMBA ZA NHC SASA KUUZWA MILIONI 17

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu, amesema shirika hilo linatarajia kuanza kujenga nyumba za gharama nafuu, ambazo zitauzwa kati ya sh. milioni 17 hadi 20.

Amesema lengo la shirika hilo ni kuwawezesha wananchi wote wenye kipato cha chini na kati, kunufaika na miradi huo, ambao umeenea nchi mzima.

Mchechu alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, wakati wa ziara ya siku moja aliyoifanya katika mikoa ya Kagera na Geita. Katika ziara hiyo, Mchechu alikagua miradi ya shirika hilo ya nyumba 40 za gharama nafuu, zinazojengwa katika wilaya za Muleba na Chato ili kuona maendeleo yake.

Alisema lengo la kuanzisha utaratibu wa kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuondoa tatizo la ukosefu wa makazi.

Mchechu alisema kila mwaka, mahitaji mapya ya nyumba ni 200,000 na kwamba, kwa Tanzania nzima uhaba wa nyumba ni milioni 3.8.

“Utaratibu wa nyumba za kupanga upo, lakini nyumba moja kama hii ikiuzwa fedha inayopataikana kwa wakati huo inawezesha kupandisha uchumi wa familia 20, ukipangisha nyumba moja faida yake inapatikana baada ya miaka 20, kwa hiyo ndio maana shirika letu limekuwa likifanya ubunifu mpya kila kukicha ili kila Mtanzania mwenye kipato chochote aweze kununua nyumba hizi za gharama nafuu,” alisema.

Aliwashauri wananchi wa Chato mkoani Geita na Muleba mkoani Kagera, kutumia fursa hiyo kununua nyumba hizo ambazo zina hati na viwanja vimepimwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuanzia Julai, mwaka huu, wanatarajia kuanzisha utaratibu mpya, ambapo wateja wanaotaka kununua nyumba, lakini hawakopesheki kwenye taasisi za fedha, wataweza kutanguliza asilimi 10 ya gharama nzima ya ununuzi wa nyumba ili kupata dhamana ya kuweza kukopeshwa.

Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera, Deogratias Batakanwa, akizungumzia utaratibu huo mpya, alisema wateja ambao wana uwezo wa kununua nyumba, lakini hawakopesheki, wakitoa asilimia 10, wanaweza kukopesheka kwa kutumia dhamana hiyo na kwamba, mteja ataendelea kurudisha mkopo huo taratibu kwa muda wa hadi miaka 20.

Alisema katika wilaya ya Muleba, wamejenga nyumba 20, ambazo zimekamilika na wilaya ya Chato kuna nyumba 20, ambazo ziko katika hatua ya mwisho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top