Rais Magufuli akimuapisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Kilango Malecel kabla ya kutengua tena uteuzi wake April 11.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezidi kumuumbua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Kilango Malecela, baada ya kusema kuwa mpaka sasa katika mkoa huo imebainika kuna wafanayakazi hewa 226.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni ambapo pia alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuweka wazi mikataba mibovu iliyosainiwa na mkurugenzi huyo.
“Nilizungumza siku ile ya kuhusu wafanyakazi hewa kule Shinyanga, mpaka leo Shinyanga kuna wafanyakazi hewa 226”, rais Magufuli alisema.
April 11 mwaka huu rais Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Kilango Malecela, baada ya kumhakikishia rais Magufuli kuwa mkoa wake haukuwa na mtumishi hewa hata mmoja, suala ambalo baadaye liligundulika si kweli kutokana na kubainika kwa watumishi hewa.
Post a Comment