RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico.
Wengine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud Talib.
Kwa upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.
Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.
Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
Post a Comment