Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU WATOA NENO UTEUZI WA ALLY SALUM HAPI KUWA MKUU WA WILAYA KINONDONI



Kwa niaba ya wana shirikisho wa CCM vyuo vya elimu ya juu Tanzania, nikiwa kama Mwenyekiti ninaye beba dhamana ya taasisi hii, kwa furaha kubwa sana nichukue fursa hii kumpongeza Mh Ally Salum Hapi kwa kuapishwa rasmi jana kuwa Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kinondoni akiwa Mkuu wa Wilaya wa 17 wa Kinondoni na kijana wa pili kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.
Kabla ya uteuzi huo, Mh Ally Salum Hapi alikuwa Mkuu wa Idara ya Elimu, Utafiti na Uongozi kwenye Shirikisho la Vyuo Vya Elimu ya Juu Taifa. Nichukue fursa hii kumshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kuwa na imani na vijana wasomi na hasa kupitia mwamvuli wa taasisi yetu kuteua Mkuu wa Wilaya nyeti na kubwa Tanzania. Taasisi hii mpaka sasa toka kurasimishwa kwake mwaka jana tumefanikiwa kutoa Wakuu wa Wilaya wawili. Naye ni aliyekuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa Shirikisho Taifa Mh Christopher Ngubiagai ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida. Na sasa Mh Ally Salum Hapi ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam. Sina wasiwasi wakati teuzi mbalimbali zikiendelea, vijana wengi kupitia mwamvuli huu watapewa nafasi.
Nilitamani kuwepo kwenye kiapo chako Mh Ally Salum Hapi, lakini kwa bahati mbaya niko kwenye ziara ya kukijenga chama nchi nzima. Hatukuwa pamoja kimwili ila kiroho tulishiriki zoezi hilo pamoja. Nakutakia kila la heri ktk utumishi wako, ukasimamie ilani ya CCM kuwatumikia wana Kinondoni na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati wowote ule, tunaahidi kukupa ushirikiano wa kutosha. Historia itakukumbuka kwa kulipigania Shirikisho hili mpaka hapa lilipo fika. Pengo lako halitazibika. Ukaongoze kwa hekima, busara, uadilifu na ubunifu.
Kasimamie haki kwa maslahi ya wana kinondoni. Tunaamini safari moja huanzisha nyingine. Tunakutabiria mema na mambo makubwa huko mbeleni. Wakati wa kuijenga serikali na sisi tunakijenga chama.

Mungu ibariki Tanzania.

Imetolewa na:
Zainab Abdallah,
M/kiti wa Shirikisho la CCM,
Vyuo Vya Elimu ya Juu Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top