Wakazi wanaoishi katika bonde la jangwani jijini dsm wameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuchukua hatua ya kupanua mito inayopita Pembeni mwa makazi yao kwa kuondoa matope ili kuepusha wakazi hao kukumbwa na mafuriko kufuatia mvua za masika zilizioanza kunyesha.
Wakizungumza na Chanel ten wakazi hao wamesema Pamoja na serikali kutawaka kuondoka maeneo hayo hatarishi ambayo hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati za Mvua wamesema hawapingi zoezi la kuondoka isipokuwa kuwepo kwa mpango wa kuwapatia makazi mengine au kupanua mito ili maji yafuate mkondo wake.
Wakati huo huo, hali ya barabara katika baadhi ya Mitaa ya kata ya Gerezani imekuwa mbaya kutokana na madimbwi makubwa yaliyotuama maji na kusababisha adha kwa watumiaji wa magari na waendao kwa miguu.
Wakizungumza na Chanel ten baadhi ya wafanyabiashara katika mitaa hiyo wameshangazwa na hali hiyo huku ikijirudia kila miaka ingawa manispaa hiyo ya ilala imekuwa ikikusanya kodi nyingi lakini miundombinu ya barabara katika eneo hilo imekuwa haipewi kipaumbele.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
Halotel yaja na mfumo wa E-SIM45 minutes ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment