Kuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao.
Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania akiwa na rappers hao. “At the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo #CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” ameandika Msando.
Kuna uwezekano kuwa nyimbo zao Usije Mjini na Dakika Moja zikawa zimetumiwa na kampuni bila ridhaa yao. Makosa ya kukiuka haki miliki kwenye kazi za sanaa huadhibiwa zaidi kwa kwa faini.
Post a Comment