Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususaniWhatsapp najua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwitaametangaza sheria mpya.
Meya Isaya Mwita ameongea na kueleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia jina lake.
“Sio kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa May 1 2016 iliripotiwa habari za mwanamke kuuwawa na mtu anayeaminika kuwa ni mpenzi wake kwa kudaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na mwanaume kuondoka kwa kumuaga mlinzi kuwa anaenda kununua vocha.
Unaweza sikiliza hapa sauti ya meya wa jiji la Dar es Salaam
Ayo
Post a Comment