Mbunge wa Handeni, Omar Abdallah Kigoda
Akitangaza matokeo hayo jana, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Tanga, Methew Mganga alimtaja Kigoda kuwa mshindi kwa kupata kura 101 kati ya 180 zilizopigwa.
Kigoda anashika nafasi iliyoachwa na baba yake, Dk Abdallah Kigoda baada ya kufariki dunia. Aliwashinda wapinzani wake Maajabu Hamis, Mussa Kidato, Athuman Lukoya na Hamis Mnondwa.
Pia, Farida Mashaka alichaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa.
Akiwashukuru wanachama, Kigoda aliahidi kufanya kazi kwa bidii bila kujali itikadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni, Athuman Malunda alisema siasa inahitaji uvumilivu na kuwataka ambao kura hazikutosha kuvunja makundi.
na badala yake wakijenge chama chao ili waweze kuisimamia serikali kwa umoja wao.
Post a Comment