WACHEZAJI saba wa Simba wakiwemo sita wa kigeni, wamegoma kusafiri kwenda Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Majimaji Jumatano.
Simba inatarajiwa kumenyana na Majimaji keshokutwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika hatua ya lala salama ya Ligi Kuu.
Na nyota wanne wa kigeni, kipa Vincent Angban (Ivory Coast), mabeki Emery Nimubona (Burundi), Juuko Murshid (Uganda), viungo Justice Majabvi (Zimbabwe), Brian Majwega (Uganda), Hamisi Kiiza (Uganda) wamegoma kusafiri.
Kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto ni mchezaji pekee anayetumia hati ya kusafiria ya nyumbani aliyegoma kusafiri na wote ni kwa sababu moja, wamecheleweshewa mishahara ya Aprili.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara, amesema kwamba sababu ya kuchelewa kuwapa mishahara wachezaji wao inatokana na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuchelewa pia kuwapatia fedha za udhamini.
Pamoja na waliogoma, Manara amesema Raphael Kiongera, Jonas Mkude, Awadhi Juma na Ibrahim Hajib nao hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa majeruhi na kutumikia adhabu za kadi.
Loading...
Post a Comment