Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI ATETEA UAMUZI WAKE WA KUWATIMUA WAFANYAKAZI


Rais John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi wa umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.

Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.

Amesema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.
 
Rais huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”,  amesema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.
 
"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top