Sakata la Sukari pamoja na operesheni zinazoendelea za kuwakamata wanaoficha Sukari limemuibua aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba na kutaka zoezi hilo lisitishwe.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho Profesa Lipumba amesema kamata kamata hiyo imesababisha wafanyabiashara kuwa na hofu, kwa madai kuwa wanashindwa kuagiza au kuhifadhi sukari jambo linalosababisha kupanda kwa bei maradufu mitaani .
Aidha Prof.Lipumba amemtaka rais Dk. John Magufuli kushirikiana na wataalamu wa Uchumi pamoja na waagizaji wa sukari ili kuangalia uwezekano kwa uagizwaji sukari kwa mfumo wa wazi ili kupunguza mianya ya rushwa au njia za panya.
Loading...
Post a Comment