Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa ni 800 na mwanafunzi 200.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’
Ayo
Post a Comment