Sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises inayomilikiwa na Said Lugumi (pichani) kudaiwa kuingia mkataba tata wa mabilioni ya shilingi wa kufunga mashine za kutambua alama za vidole kwenye vituo vya polisi nchini, limeingia mitaani huku baadhi ya Wabongo wakitaja njia 3 za kumaliza ishu hiyo.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walionesha shaka yao kuhusu sakata la Lugumi kuwa gumzo likiumiza vichwa vya wabunge kama vile mhusika amekwenda Ulaya, hivyo wakatoa maoni yao.Shida Waziri, mkazi wa Ubungo External, Dar alisema: “Lugumi mwenyewe tunaambiwa hayupo mbali, anaendelea kuishi kwa amani hapahapa Tanzania. Mimi nashauri aitwe, ahojiwe mbele ya jopo la watu maalum, wakiwemo Usalama wa Taifa.“Hii itasaidia sana kwani ataweza kuanika kila kitu. Mkataba ulivyokuwa, ulivyokwenda, nani na nani walihusika.”John Joseph, mkazi wa Kigogo, Luhanga, Dar: “Mimi nashauri serikali iunde jopo nje ya wabunge, ila wawepo Usalama wa Taifa. Wapite kituo hadi kituo cha polisi na kutaka kuziona kwa macho hizo mashine, basi.“Baada ya siku kumi na nne tu jopo litajua kituo gani kilifungwa, kituo gani hakikufungwa. Maana tunahisi kuna mzunguko mkubwa pasipo sababu.”Mwanahawa Ally, mkazi wa Ilala, Dar: “Njia pekee ya kumaliza sakata la Lugumi ni kuwaita wachunguzi wa kimataifa kama wale New Scotland Yard ya Uingereza. Wale ni wapelelezi wa kila jambo hata liwe la siri kwa kiasi gani.“Wamebobea katika kuchunguza shaka yoyote ile. Kwa hiyo naamini wakitumika wale wanaweza kuleta majibu. Huwa wanaitwa katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchunguza mambo magumu.”Wakati huohuo, baadhi ya wananchi wamesema hawaoni sababu ya baadhi ya wabunge kumsakama Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa anahusika na mkataba wa Lugumi bila kuweka ushahidi usio na shaka.“Mimi nawasikia wabunge wakisema Kitwanga ajitetee sakata la Lugumi. Ajitetee nini wakati ushahidi wenyewe wanaouweka ni wa kuungaunga tu. Hata Mahakama haihukumu jambo bila kupata ushahidi usio na shaka,” alisem Jumanne Mshindo, mkazi wa Buguruni, Dar.TUJIKUMBUSHEMwaka 2011, Kampuni ya Lugumi ilipewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini ambapo inadaiwa imeshalipwa Sh. bilioni 34 kati ya bilioni 37, sawa na asilimia 99 ya malipo yote.Hata hivyo, kuna madai kwamba ni vituo 14 tu vilivyofungwa mashine hizo huku mashine moja pekee ikiwa ndiyo inayofanya kazi.Vifaa hivyo vingeweza kutambua alama za vidole kwa wahalifu hasa wale wanaofanya uhalifu sehemu moja na kukimbilia nyingine.Kufuatia sakata hilo, Aprili 21, mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aeshi Hilary aliunda kamati ndogo yenye wabunge tisa, kuchunguza kwa kina mkataba huo na kupewa siku 30 za kufanya kazi hiyo kisha taarifa itatolewa bungeni.Kamati hiyo itawahoji mawaziri, viongozi wa jeshi la polisi waliopo na waliostaafu, wafanyabiashara waliotajwa pamoja na kampuni zilizoshiriki kufunga mashine hizo.
on Thursday, May 19, 2016
Post a Comment