Derick Lwasye, Mbeya
KLABU ya Yanga imepanga kufanya mabadiliko ya kulitumia basi lao ambalo walipewa na wadhamini wao Kampuni ya Bia (TBL) ambapo litakuwa maalum kwa mashabiki wao badala ya kutumiwa na wachezaji wao.
KLABU ya Yanga imepanga kufanya mabadiliko ya kulitumia basi lao ambalo walipewa na wadhamini wao Kampuni ya Bia (TBL) ambapo litakuwa maalum kwa mashabiki wao badala ya kutumiwa na wachezaji wao.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alipokuwa kwenye uzinduzi wa Tawi la Yanga Uswazi Mbeya eneo la Sokomatola juzi Jumatano wakati Yanga ilipokuwa jijini hapa kucheza na Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Muro amesema uamuzi huo wameufikiria kwa kuwa wamekuwa wakitumia zaidi usafiri wa ndege ambao umezaa jina la wao kuitwa wa kimataifa pamoja na kushiriki michuano ya nje.
“Sisi ni watu wa angani tu muda wote, hivyo hata basi letu tumepanga kuwapa mashabiki walitumie kwa ajili ya kusafiri kuifuata timu kuipa sapoti, wale ndugu zetu wao ndiyo wa kutumia basi.
“Kwa mfano sisi tumeingia hapa asubuhi, tumetoka Dar saa 12 asubuhi, saa moja tumetua hapa, ila watani waliondoka Dar, jana asubuhi hadi leo (juzi) hawajafika Songea,” alisema Muro huku akishangiliwa na mashabiki wa Yanga waliokuwa eneo hilo.
“Msimu ujao pia tutashiriki katika michuano ya kimataifa, hivyo muda mwingi tutakuwa na safari za nje kama ilivyo msimu huu, hivyo hili basi letu litakuwa linatumika kuwafuata mashabiki na kuwapeleka mkoa mwingine pindi sisi tutakapokuwa tunasafiri kwa ndege,” aliongeza Muro.
Alisema kuwa ikiwa uamuzi huo utapitishwa, basi wao watakuwa wanasafiri kwa ndege tu hata katika safari za ndani na basi lao litakuwa linatumiwa na wachezaji katika safari za ndani ya Dar tu.
Post a Comment