Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWSS ... ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA JELA MIAKA 3 AU KULIPA FAINI YA MILIONI 7

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu  Isack Habakuki(40) mkazi Wa Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa facebook. 

Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili. Katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5. 

Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile,  Wakili wa Serikali, Gaudensia Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Magufuli.

Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top