Kurasa hizo zimekuwa zikitumiwa na mamia ya watu katika kupanga bajeti zao binafsi kabla ya kuamua kufanya manunuzi ya bidhaa hasa magari nje ya nchi.
Ili kuweza kukokotoa kiasi halisi cha kodi ambacho TRA wanaweza kukukata kabla ya kumua kuagiza gari ililotumika kutoka nje ya nchi, tembelea tovuti ya TRA kipingere cha Quick Links na hapo chagua Calculators & Tools au unaweza ukabonyeza hapa.
Utaletewa fomu ya kujaza taarifa za gari unaotaka kuagiza kama aina ya gari, kampuni iliyotengeneza, aina ya bodi, mwaka wa iliotengenezwa na nchi unapotaka kuiagiza, uwezo wa injini na mafuta.
Hapa kitu cha muhimu zaidi kukifahamu ni mwaka ambao gari limetengenezwa na uwezo wa injini (Engine Capacity (cc)). Kodi huongezeka zaidi kulingana na mwaka ambao gari limetengenezwa, gari linapozidi kuwa la zamani na kiasi cha kodi huongezeka maradufu, hii ni kuendana na sera za nchi yetu na sera za kimazingira ili kupunguza idadi ya magari mabovu yanayoagizwa nchini.
Post a Comment