Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAGARI YALIYOSAMEHEWA KODI KUWEKEWA NAMBA MAALUM

Dodoma. Serikali imeweka masharti mapya kuhusiana na misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini, ikiwamo magari yatakayoagizwa na kusamehewa kodi kuwekwa namba maalumu.

Uamuzi huo wa Serikali unafuta ule wa awali wa kuzitaka taasisi za dini kulipa kodi kwanza, na baadaye ndiyo kuomba msamaha.

Wakati akisoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2016/17,  Juni 8, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipendekeza kufuta misamaha hiyo na kwamba taasisi za kidini zingetakiwa kulipia kodi vifaa wanavyoingizwa nchini na kurudishwa fedha zao zilizotumika kama kodi baada ya Serikali kujiridhisha kuwa vifaa husika vilitumika ipasavyo.

Lakini jana, Dk Mpango aliwaeleza wanahabari ofisini kwake kuwa baada ya kupokea maoni kutoka kwa wabunge na wadau mbalimbali kuwa utaratibu aliokuwa amependekeza umeonekana ungeweza kukwamisha au kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya taasisi za kidini na kusababisha athari katika upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha hiyo, Dk Mpango alisema taasisi hizo kwa sasa kila Januari zitatakiwa kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa na kuthibitisha kama vifaa walivyopatiwa msamaha mwaka uliopita vilitumika ipasavyo.

“Zitatakiwa kuwasilisha majina ya watu walioidhinishwa na shirika au taasisi kuomba misamaha ya kodi huku wakianisha vyeo, saini, picha, anuani zao na namba za simu ili iwe rahisi kuwafikia,” alisema.

Alisema taarifa hizo zitaisaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujua iwapo watu wanaoomba misamaha wamepatiwa kibali kwa kuwa imetokea baadhi ya watu wanaoomba misamaha hiyo hawajulikani hata na Askofu wala Sheikh Mkuu au viongozi wa juu wa taasisi husika.

Dk Mpango alieleza kuwa kila wanapoomba misamaha hiyo wanapaswa kupata barua kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa na Mkuu wa wilaya ambako mradi unafanyika kuthibitisha uwepo wa mradi au taasisi inayoombewa msamaha.

“Magari yanayoagizwa kwa msamaha yawe na namba na rangi maalumu za utambuzi mfano; TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake,” alisema Dk Mpango akieleza kuwa kila taasisi inapaswa kuandika barua kumuidhinisha wakala wa forodha waliomteua kutoa mizigo bandarini.

Alisema kuwa kuna baadhi ya taasisi hizo hazina uwezo wa kutoa kodi hiyo ya awali, kwa kuwa wanatambua umuhimu wao katika utoaji wa huduma za afya na elimu, anapendekeza kufuta utaratibu aliokuwa ameutangaza awali.

Mabadiliko hayo yapo kwenye Muswada wa Fedha uliopitishwa juzi na Muswada wa Matumizi utakaowasilishwa leo bungeni.

Kuhusu kodi ya majengo kukusanywa na TRA, alisema atashauriana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, George Simbachawene juu ya viwango vya utozaji na kodi hizo zitatozwa kwa kuzingatia eneo na nyumba husika baada ya kupata maoni ya wadau zikiwamo halmashauri.

“Naomba niwambie Watanzania kuwa utawala huu ni wa kulipa kodi. Hatuwezi kumuacha mwenye nyumba aweke mfukoni kodi yote halafu aende kudai huduma bora hospitalini. “Niwahakikishe kuwa tutaanza na viwango vya kodi rafiki vinavyolipika na mwananchi wa kawaida na hii itatusaidia kubaini umiliki wa nyumba nchini,” alisema.

Akielezea kuhusu asilimia 10 ya kodi ya bidhaa katika miamala ya fedha za simu za mkononi, Dk Mpango alisema Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kushirikiana na Benki Kuu (BoT) na TRA kuhakikisha tozo hiyo inaendana na uhalisia wa huduma inayotolewa.

Alisema pia TCRA itafanya ukaguzi wa kina katika miamala ya kampuni za simu kabla na baada ya tozo ili yasihamishie mzigo kwa wananchi.

“Napenda nizieleze benki na kampuni za simu kuwa mzigo huo ni wa kwao na si wa wananchi,” alisema Dk Mpango.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top