Jacqueline Wolper Massawe na mkwe wake, mama Harmonize.
DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa wa Wimbo wa Bado, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumtambulisha mchumba’ke, Jacqueline Wolper Massawe nyumbani kwao katika Kijiji cha Mahuta mkoani Mtwara, siri imevuja kuwa wakati wa zoezi hilo, mama mzazi wa jamaa huyo, anadaiwa kumtilia shaka mrembo huyo juu ya mwanaye na kumpa wosia mzito.
Tukio la utambulisho huo lilifanyika nyumbani kwa akina Harmonize Mtwara mara baada ya jamaa huyo kutinga mkoani humo kwa shoo yake ya kwanza maeneo hayo tangu alipochomoka kimuziki.
Ilielezwa kwamba, akiwa katika harakati hizo mapema siku ya tukio, Harmonize alikwenda nyumbani kwao na kumtambulisha Wolper kisha usiku wake akampandisha mama yake kumtambulisha kwa mashabiki na baada ya kumtambulisha Wolper ambaye ni staa wa Bongo Muvi.
Rajab Abdulhan ‘Harmonize’na mama yake mzazi.
“Kiukweli Wolper amekubalika kwa mama Harmonize ila mzazi huyo alionesha shaka kama kweli Wolper ataweza kuishi na mwanaye maana alidai mastaa wengi wa kike huwa hawadumu kwenye uhusiano wa kimapenzi, hivyo alionesha kuwa shaka kama kweli Wolper atakuwa na nia njema na mwanaye au yupo kwa ajili ya kuchota vijisenti kisha ammwage kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanyiana,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Wikienda lilimsaka Harmonize ili kujua kama kweli mama yake alimkubali Wolper au alionesha shaka naye kama chanzo chetu kilivyotonya. Msanii huyo aliliambia gazeti hili kuwa kwa namna moja au nyingine mama yake alimpokea mpenzi wake huyo kwa moyo mkunjufu japokuwa aliwahusia kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila jambo.
“Mama alimpokea vizuri sana kiasi kwamba hata mimi nilibaki nikishangaa kwani alimpenda na hata kufikia hatua ya kututaka tuendelee kuheshimiana kwa kila hali kwani njia pekee ya kufika mbali ni kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila jambo japokuwa kwenye maisha ya kila siku kukwaruzana hakuepukiki,” alisema Harmonize.
Kwa upande wake Wolper aliliambia gazeti hili kuwa kwenye maisha hakuna raha kama kuishi kawaida kwa sababu ukawaida ndiyo ulimfanya kukubalika kwa mama Harmonize.
“Hayo ni maneno ya watu lakini alifurahia sana staili yangu ya kuishi kawaida maana kama ningekuwa na tabia ya kujiona staa basi watu wasingeweza kunizoea na kunikubali kama ilivyokuwa kwa mama mkwe,” alisema Wolper.
Wolper na Harmonize walianza uhusiano wa kimapenzi hivi karibuni huku wengi wakidhani kuwa ni ‘kiki’ kabla ya mambo kukolea na sasa uhusiano wao umegeuka habari ya mjini.
Post a Comment