Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni Boniface Jacob akizungumza na Mafisa Watendaji juu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kuwafukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.
HALMASHAURI ya Manispaa ya kinondoni imefukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.
Akizungumza leo na maafisa watendaji kata, meya wa kinondoni boniface jacob amesema kuwa hawatavumilia watendaji wanaofuja fedha za umma.
Watendaji waliofukuzwa ni Ernest Misa na Ally Bwanamkuu na wengine wawili wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi ambao ni Shaban Kambi pamoja na Bernard Supu.
Aidha Meya huyo amesema zipo kata tano ambazo zimekusanya mapato vizuri na kata tano zingine zimefanya vibaya hivyo wanatafuta dawa ya kuwaondoa watendaji waliofanya vibaya.
Jacob amesema migogoro ya ardhi imepungua kutokana na kila watendaji kuwajibika katika zao awali migogoro ilikuwa inasababishwa na wenyewe
Amesema kinondoni wanataka kuibadili katika kuhakikisha watendaji wanawahudumia wananchi kuachana kufanya kwa mazoea.
Loading...
Post a Comment