Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob Boniface akisaini mkataba wa kutengeneza madawati na Mkurugenzi wa Kampuni ya Edosama Hardware, leo jijini Dar es Salaam.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mkataba na wazabuni 10 wa kutengeneza mdawati 28000 leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliokuwa wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa kutengeneza madawati wa shule za msingi na Sekondari katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imekata posho za watendaji wa idara zake kwa muda wa miezi miwili na kuweza kupata sh.bilioni 1.8 ambazo zitamaliza tatizo la madawati 28000 kwa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Kinondoni.
Kuondosha kwa posho hizo kulitokana na manispaa kubaini kuwa hawana uwezo wa kununua madawati 28000 kwa kukosa bajeti hiyo katika mwaka fedha 2015/2016 na kuona posho za watumishi zitumike kununua madawati hayo.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mkataba wa kampuni 10 za kutengeneza madawati 28000, Meya wa Manispaa Kinondoni, Jacob Boniface amesema kuwa kwa kuingia mkataba huo kinondoni inachana na tatizo la madawati.
Jacob amesema kuwa Kinondoni wanafunzi kukaa chini ni aibu kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na vyanzo mapato vingi.
Amesema kuwa waliongia mikataba kuhakikisha kufikia juni 30 mwaka huu wazabuni wote kuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati.
Jacob amesema kuwa madawati yanayokusanywa na wadau mbalimbali wanayahitaji kwa ajili kuweka akiba ili yakiharibika kuweza kutumika pale penye upungufu.
Ameasema madawati hayo yanatengenezwa kwa bei ndogo kuliko na awamu zote kwani kwa sasa yanatengenezwa kwa sh.85000, wakati kwa manispaa hiyo ilishatengeneza dawati moja kwa sh.400,000.
Post a Comment