Na mwandishi wetu
RISASI MCHANGANYIKO
MASTAA mbalimbali wa filamu na muziki, leo wanatarajiwa kufaidika kwa kupata chanzo kingine cha mapato baada ya kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, kutangaza uzinduzi wa ‘project’ mpya iitwayo Staa Wako.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Martina Nkuru, mpango huo utawahusu mashabiki wa mastaa hao, ambao watapata habari zao moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi.
“Kama mtu ni shabiki wa staa kama Lady Jaydee kwa mfano, akihitaji kupata habari za msanii huyo, anajiunga kwa namba ambazo tutawapatia na kuanzia hapo, atapata habari zake kadiri zinavyotokea. Kama anafanya uzinduzi wa nyimbo, video au shughuli yoyote, unakuwa wa kwanza kupata habari zake moja kwa moja,” alisema Nkuru.
Aliwataja mastaa ambao wameingia mkataba na kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi kuwa ni Lady Jaydee, Alikiba Saleh, Aunty Ezekiel, Kajala Masanja, Jacqueline Wolper, Shilole na Rose Ndauka.
Post a Comment