Kuna makala moja ya kisayansi nilikua naipitia leo na nikashangazwa kugundua kwamba mnyama mkubwa zaidi aliyewahi kuishi duniani anaitwa Giraffatitan.
Huyu mnyama aliishi jurrasic era takribani miaka milioni 150 iliyopita na inasemekana uzito wake ulikua unafika tonne 80 na urefu wake zaidi ya metre 20.
Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba huyu mnyama mabaki yake ikijumuisha fuvu lake yaligundulika Lindi, Tanzania kipindi cha utawala wa kikoloni wa wajerumani hapo mwaka 1909 na 1912.
Mabaki yake sasa yametundikwa Berlin, Ujerumani na yamekua ni kivutio kikubwa cha utalii nchini kule.
Kwanini sasa serikali na wizara inayohusika na utalii wasianzishe kampeni na mijadala ya mabaki ya mnyama huyu kurudishwa Tanzania kwasababu alichukuliwa kwa njia ambayo siyo halali.
India na nchi nyingine wameweza kupigania mali nyingi zilizoibwa kipindi cha ukoloni zirudishwe na zimerudishwa kwanini sasa Tanzania tusiige mfano.
Tanzania ikumbukwe ndo craddle of all civilization, binadamu wa kwanza wameishi hapa miaka milioni iliyopita na wanyama wenye super genes kama. huyu wameishi hapa pia. Ombi langu serikali ifanye jitihadi kurudisha mabaki ya huyu mnyama na wengine wengi. Itakuza utalii wa ndani na kurudisha sense of National Pride ya kujivunia kuwa Mtanzania.
Loading...
Post a Comment