JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TELEGRAMS: POLISI, OFISI YA
TELEPHONE: 2500712 KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310 MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com S.L.P.120,
rpc.mwanza@tpf.go.tz MWANZA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
• MWANAMKE MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA WILAYANI MAGU.
• MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA MNAMO TAREHE 08.06.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA MAKALE KIJIJI CHA KAYENZE B KATA YA NKUNGURU TARAFA YA NDAGULA WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA , MARIAM NHABAGULA MIAKA 33 MKAZI WA KAYENZE B ALIKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFARIKI PAPO HAPO KWENYE MTI KWA KUTUMIA KAMBA YA KATANI.
INADAIWA KUWA MAREHEMU KABLA YA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUJINYONGA ALIKWENDA KUPIMA AFYA YAKE NDIPO ALIPOKEA MAJIBU KUWA NIMUATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI, HALI ILIYOPELEKEA KUAMUA KUJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA.
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI JUU YA TUKIO HILO ILI KUWEZA KUJIRIDHISHA JUU YA MADAI YA KIFO HICHO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMEWATAKA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KUISHI KWA UPENDO NA USHIRIKIANO PAMOJA NA KUFARIJIANA KATIKA KILA HALI, ILI KUWEZA KUZUIA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA KATIKA JAMII ZETU.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 09.06.2016 MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA MTAA WA LIBERTY KATA YA PAMBA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO NA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA MATONDO JAMES MIAKA 39 MKAZI WA IGOMA AKIWA NA PAKITI MOJA [01] YA MADINI YAZANIWAYO KUWA NI BANDIA WAKIYATUMIA KUTAPELI WATU KATIKA MITAA BARABARANI NA KWENYE MABENKI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, NA TAYARI WATU WENGINE WATATU AMBAO MAJINA YAO YAMEHIFADHIWA WAMEKAMATWA HIVI PUNDE NA JESHI LA POLISI WAKIHUSIANISHWA KUSHIRIKIANA NA MTUHUMIWA KATIKA KUFANYA UHALIFU HUO KATIKA JIJI LA MWANZA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA KAZI YA KUWATAPELI WAPITA NJIA NA WATEJE WA MABENKI KUWA WANAUZA MADINI, HIVYO HUWAAMBIA WANAUZA MADINI YA AINA YA ZAHABU NA MARA NYINGINE HUWAANBIA WANAUZA ALMASI LAKINI KIPINDI HICHO WANAKUWA WAMEYAFUNGA MADINI HAYO BANDIA KWENYE PAKITI NA HUMSHAWISHI MNUNUAJIA AKAIFUNGUE PAKITI HIYO YENYE MADINI SEHEMU WANAPO NUNUA MADINI, PINDI MPITA NJIA AKIKUBALI KUUZIWA MADINI HAYO ANAKUWA TAYARI WAMEMTAPELI NA MATAPELI HAO HUTOROKA MUDA HUO MAHALI WALIPOFANYA UHALIFU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUWEZA KUWAKAMATA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTAPELI WA AINA KAMA HIYO NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, LAKINI PIA AKIWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA MTU AU WATU WANAOZANIWA KUWA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Post a Comment