Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Zackaria Mswaki (pichani) amehukumiwa na mahakama ya mwanzo Mlalo lushoto mkoani Tanga kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa akiuza nyama ya Mbwa ambapo asilimia kubwa ya watu katika mji huo mdogo uliopo wilaya ya lushoto walinunua nyama hiyo na kula bila wao kujua. mshtakiwa amekiri shtaka mbele ya mahakama na kudai ugumu wa maisha ndio chanzo cha kufanya hivyo mshatakiwa amepelekwa Gereza la wilaya lushoto kutumikia adhabu Yake huku akiwa amewaacha wananchi wa mji huo na butwaa pamoja na hasira ya kuwalisha nyama ya mbwa
on Wednesday, June 1, 2016
Post a Comment